Thursday 14 January 2016

ZIFUATAZO NI FAIDA YA DAGAA KATIKA MWILI WAKO

AFYA YA MIFUPA

Dagaa ni chanzo kingine kizuri cha madini ya ‘Calcium’ yenye jukumu la kuimarisha mifupa ya mwili, lakini pia kwenye dagaa kuna vitamin D ambayo huwa nadra sana kupatikana kwenye lishe.

Vitamin D hufanyakazi muhimu ya kuimarisha afya ya mifupa kwani ndiyo inayosaidia unyonywaji mwilini wa madini ya ‘calcium’. Vile vile dagaa ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘phosphorus’, ambayo nayo huimarisha mifupa.


DAGAA NA KANSA

Kwa miaka mingi, watafiti wameona jinsi ambavyo dagaa inavyoweza kudhibiti seli zinazosambaza saratani mwilini. Hivyo imethibitika pasi na shaka kuwa virutubisho vilivyomo kwenye dagaa huweza kutoa kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wa saratani.


WAMEJAA PROTINI

Kama una upungufu wa protini mwilini, basi kula dagaa kwani wao wana kiwango kikubwa cha kirutubisho hicho. Protini husaidia uzalishaji wa ‘Amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa chembe hai mwilini na uimarishaji wa mfumo wa kinga ya mwili (body immune system).

0 comments:

Post a Comment

Whasapp tunapatikana kwa 0687599999 au piga simu 0714584583 www.instagram.com/doubletfood