Monday 18 January 2016


Saturday 16 January 2016

Thursday 14 January 2016



ZIFUATAZO NI FAIDA YA DAGAA KATIKA MWILI WAKO

AFYA YA MIFUPA

Dagaa ni chanzo kingine kizuri cha madini ya ‘Calcium’ yenye jukumu la kuimarisha mifupa ya mwili, lakini pia kwenye dagaa kuna vitamin D ambayo huwa nadra sana kupatikana kwenye lishe.

Vitamin D hufanyakazi muhimu ya kuimarisha afya ya mifupa kwani ndiyo inayosaidia unyonywaji mwilini wa madini ya ‘calcium’. Vile vile dagaa ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘phosphorus’, ambayo nayo huimarisha mifupa.


DAGAA NA KANSA

Kwa miaka mingi, watafiti wameona jinsi ambavyo dagaa inavyoweza kudhibiti seli zinazosambaza saratani mwilini. Hivyo imethibitika pasi na shaka kuwa virutubisho vilivyomo kwenye dagaa huweza kutoa kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wa saratani.


WAMEJAA PROTINI

Kama una upungufu wa protini mwilini, basi kula dagaa kwani wao wana kiwango kikubwa cha kirutubisho hicho. Protini husaidia uzalishaji wa ‘Amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa chembe hai mwilini na uimarishaji wa mfumo wa kinga ya mwili (body immune system).

Wednesday 13 January 2016

Package yake iko bora kwa mtumiaji kwakuwa unaweza kutumia na ukafunga kwa matumizi ya baadae, Double T food imeandikwa hvyo kwa kumanisha 'TASTE TASTY" maneno hayo yakiwa na maana ya "RADHA TAMU" ni uzuri ulioje kupata kula chakula kitamu tena kisicho na usumbufu, ungana nasi sasa.


  • Andaa kitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti. Osha, kata vipande vidogo tayari kwa mapishi.
  • Andaa tui la nazi – vunja nazi, kuna na kisha kamua tui zito na hifadhi vizuri pembeni.
  • Weka sufuria ya kupikia jikoni, kisha mimina mafuta ya kula kiasi. Subiria yapate moto vizuri.Weka vitunguu kwenye sufuria.
  • Koroga mpaka vianze kubadilika rangi kidogo.
  • Vitunguu vikianza kubadilika rangi, weka dagaa wa double T. Koroga na kukaanga vizuri dagaa wa double T kwa muda wa dakika chache.Dagaa wa double T wakianza kukauka 
  • kamulia ndimu au limao juu yake. Koroga kiasi kisha weka pilipili hoho na karoti. Endelea kukoroga.
  • Weka nyanya kwenye dagaa. Endelea kukoroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziive vizuri na mvuke na kuwa laini.
  • Nyanya zikiiva unaweza kuziponda ili kupata rojo nzuri...pia unaweza kuongeza tomato paste kama nyanya chache au mbichi...
  • Weka chumvi unayoona inafaa kutokana na kiwango cha mboga.