Andaa kitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti. Osha, kata vipande vidogo tayari kwa mapishi.
Andaa tui la nazi – vunja nazi, kuna na kisha kamua tui zito na hifadhi vizuri pembeni.
Weka sufuria ya kupikia jikoni, kisha mimina mafuta ya kula kiasi. Subiria yapate moto vizuri.Weka vitunguu kwenye sufuria.
Koroga mpaka vianze kubadilika rangi kidogo.
Vitunguu vikianza kubadilika rangi, weka dagaa wa double T. Koroga na kukaanga vizuri dagaa wa double T kwa muda wa dakika chache.Dagaa wa double T wakianza kukauka
kamulia ndimu au limao juu yake. Koroga kiasi kisha weka pilipili hoho na karoti. Endelea kukoroga.
Weka nyanya kwenye dagaa. Endelea kukoroga na kisha funika na mfuniko ili nyanya ziive vizuri na mvuke na kuwa laini.
Nyanya zikiiva unaweza kuziponda ili kupata rojo nzuri...pia unaweza kuongeza tomato paste kama nyanya chache au mbichi...
Weka chumvi unayoona inafaa kutokana na kiwango cha mboga.
0 comments:
Post a Comment
Whasapp tunapatikana kwa 0687599999 au piga simu 0714584583 www.instagram.com/doubletfood